Siku hizi kulaumu na kulalamika imekuwa ni kama jambo la kawaida miongoni mwa jamii zetu, ni kawaida kuona tunailaumu na kuilalamikia serikali na viongozi wake, kuyalalamikia mazingira na vingine kama hivyo,Sijaribu kuwatetea viongozi wetu, mazingira na vingine ambavyo vimekuwa vikilalamikiwa kama chanzo cha matatizo ni kweli kabisa wanaolalamikiwa wanafanya tofauti na vile ilivyotakiwa kufanyika, lakini je kuendelea kukaa na kulaumu kumesaidia kuondoa matatizo?Wahenga walisema “kelele za chura hazimzuii tembo kunywa maji” ndio maana siku zote tumekuwa tukilaumu na kulalamika lakini mambo yapo vile vile.Kuna mambo mawili makubwa yapaswa tujifunze ili tuwe na Uwezo wa kubadilisha hali isiyohitajika na kuitengeneza hali inayohitajika,1.Moja ya sifa kubwa ya mtu anaeyaona na kugundua matatizo anatakiwa awe na uwezo wa kujua suluhisho la matatizo hayo hivyo tuondokane na tabia ya kulaumu na kulalamika na tutengeneze kitu kinachoitwa KUKOSOA KUNAKOJENGA ( CONSTRUCTIVE CRITICISM) Kuna mtu mmoja aliwahi kusema “DON’T END UP BY SAYING THIS SHOULD NOT BE DONE GO FURTHER BY SAYING WHAT SHOULD BE DONE INSTEAD” akimaanisha usiishie kusema jambo hili halikutakiwa kufanyika nenda mbele zaidi na kusema jambo lililotakiwa kufanyika kama mbadala wake. Badala ya kuyalalamikia makosa yanayofanywa tunatakiwa tuyakosoe kwa kushauri nini kifanyike ili mambo yaende sawa.2.Tambua wewe ndiye mabadiliko yenyewe yanayosubiliwa, Dr Myles Munroe aliwahi kusema “YOU CAN’T CHANGE SOMETHING WHICH YOU NEVER ENGAGE IN” akimaanisha hauwezi kubadilisha kitu ambacho wewe mwenyewe haujaingia ndani yake. Hivyo basi wewe ambaye unaona wengine wanafanya tofauti unatakiwa utafute na kuingia katika sehemu hiyo na kutenda kwa usahihi ili uwaonyeshe wengine jinsi inavyotakiwa kufanyika ili wajifunze kutoka kwako na wafanye sawasawa na itakiwavyo kufanyika. Rais wa Marekani mheshimiwa Barrack Hussein Obama aliwahi kusema ” MABADILIKO HAYAWEZI KUJA IWAPO TUTASUBIRI MTU MWINGINE AU TUTASUBIRI WAKATI MWINGINE, SISI NI WATU TULIOSUBILIWA SISI NDIO MABADILIKO YANAYOTAFUTWA”.Jifunze kuwa sababisho la mabadiliko, hakikisha wengine wanabadilika kwa sababu yako.Tambua, Si rahisi kubadilisha na wengi hupinga mabadikiko, anza na Mungu, tembea naye katika njia zako, maliza Naye, BILA MUNGU HAUWEZI KUFANYA CHOCHOTE.

Tazama hapa ujifunze namna ya kuacha kulalamika kisa kitu fulani huna.

Dr.Japhet Simon

Inspirational Speaker|Author|Business Consultant|Entrepreneur|Blogger

Facebook:Japhet K.Simon

Instagram;japhetsimon_

Published by Dr.Japhet Simon

Inspirational Speaker|Author|Tutor|Business Consultant|Entrepreneur|Blogger

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create your website with WordPress.com
Get started
%d bloggers like this: